Wanajeshi wa Iraq wamefika katikati mwa mji wa Baiji hapo jana katika juhudi za kuutwa kutoka mikononi mwa magaidi wa Daesh. Kusonga mbele kwa wanajeshi wa Iraq katika mji huo ulio na kiwanda kikubwa zaidi cha kusafishia mafuta nchini Iraq, kumetokana na ushindi baada ya mapigano makali kati ya magaidi hao wa Daesh na wanajeshi hao.Kwa upande mwingine kuna ripoti za kuhitilifiana kuhusu kifo cha Abu Bakr al Baghdadi ambaye ni kiongozi wa magaidi wa Daesh, ambapo anasadikiwa kuuawa baada ya mashambulizi ya angani yanayoongozwa na Marekani kuzishambulia ngome mbili na msafara wa magaidi hao nchini humo, ambako inasadikiwa kuwa Al Baghdadi alikuwepo katika msafara huo ulioshambuliwa.
Pia kumeripotiwa mafanikio ya jeshi la Iraq wakishirikiana na jeshi la wananchi waliojitolea, ambapo wamewaangamiza magaidi kadha wa kadhaa katika miji mbalimbali.
10 Novemba 2014 - 11:10
Msimbo wa Habari: 650458
Wanajeshi wa Iraq wamefika katikati mwa mji wa Baiji hapo jana katika juhudi za kuutwa kutoka mikononi mwa magaidi wa Daesh.